Tuesday, May 26, 2009

J.Kaseja huyoo Msimbazi tena

Blog hii imefahamishwa kwamba Juma Kaseja amesaini kuchezea Simba msimu ujao. Kaseja (pichani akisaini mkataba wa kuchezea Yanga mwaka jana) amekubali kuchezea Simba si kwa sababu ya pesa alizopewa tu, bali pia kutokana na mapenzi aliyonayo kwa timu hii. Ieleweke kuwa usajili wa mwaka huu zimeongezeka timu 2 zinazotumia pesa nyingi katika usajili, Azam (Ya Bakhresa) na African Lyon (Ya Moh'd Enterprises) ambazo zote zilikuwa zikimtaka kaseja pia. Katika hatua nyingine, Mganga wa tiba Asili (Maji Marefu) amejitolea kumlipa Kaseja 1.5M kama mshahara kila mwezi.

4 comments:

  1. je havari hizi ni zauhakika au ni tetesi tu.Mimi ni mpenzi mkubwa wa Simba nisingependa utupe habari amabazo sio za uhakika kwa asili mia miamoja.Naomba utupe confirmation ya habari hizi.Nimesikia kwamba Amri Kiemba nae kasaini.Inaelekea una mawasiliano na watu wa usajili hivyo tupe habari moto moto.

    ReplyDelete
  2. Amri Kiemba iko confirmed kuwa ame sign. Unajua tatizo la usajili kuna trick nyingi, inawezekana kiongozi aliyenipa habari hii amefanya hivi kuwakatisha tamaa timu zinazomfatilia (ambayo ni mbinu inayokubalika). Habari nyingi zinazowekwa hapa zinatoka ktk zource za ndani ya club, lakini sio official maana hii sio official Team blog. From Blogger

    ReplyDelete
  3. Amri Kiemba iko confirmed kuwa ame sign. Unajua tatizo la usajili kuna trick nyingi, inawezekana kiongozi aliyenipa habari hii amefanya hivi kuwakatisha tamaa timu zinazomfatilia (ambayo ni mbinu inayokubalika). Habari nyingi zinazowekwa hapa zinatoka ktk zource za ndani ya club, lakini sio official maana hii sio official Team blog. From Blogger

    ReplyDelete
  4. Amri Kiemba iko confirmed kuwa ame sign. Unajua tatizo la usajili kuna trick nyingi, inawezekana kiongozi aliyenipa habari hii amefanya hivi kuwakatisha tamaa timu zinazomfatilia (ambayo ni mbinu inayokubalika). Habari nyingi zinazowekwa hapa zinatoka ktk zource za ndani ya club, lakini sio official maana hii sio official Team blog. From Blogger

    ReplyDelete