Wednesday, August 12, 2009

Tumepata Uzi wa mwaka,lakini.....

Naupongeza uongozi wa Simba kwa kutoa jezi za mwaka iliwashabiki wafurahi kuvaa jezi za timu yao na mapato ya timu kuongezeka. Lakini, hivi tumeshindwa kuweka nembo ya timu yetu na tangazo la wadhamini? Hivi ukikuta duka linauza jezi kama hizi bila ruhusa ya klabu utaweza kuwashtaki? na wadhamini hamuoni nao wanahitaji kuungwa mkono kwa kuweka tangazo lao ktk jezi hizi?

Saturday, August 8, 2009

Simba Day yafana, Villa yapigwa 1 - 0

Tamasha la Simba Sports Club day limefanyika leo na kufana vilivyo. Tamasha hilo lililotanguliwa burudani ya muziki, utambulisho wa wachezaji na jezi za msimu lilimaliziwa kwa mechi kati ya Sima na SC Villa ya Uganda. Katika mechi hiyo Simba iliilaza Villa kwa bao 1 - 0 lililowekwa kimiani na mchezaji mpya wa simba aliyesajiliwa kutoka SC VIlla, Hillary Echesa

Ama kweli msimu huu utakuwa moto!

Tuesday, August 4, 2009

Kwa taarifa yako!

Timu ya Simba Sports Club lipoanzishwa mwaka 1936, ilikuwa inaitwa QUEENS. Chukua hiyo shabiki wa msimbazi.

Friday, July 31, 2009

Simba sasa kama Ulaya

Uongozi wa Simba umefungua kurasa mpya ambapo kuanzia msimu huu, kutakuwa na jezi za msimu. Jezi hizo zitatambulishwa tarehe 8/8 katika siku itakayoitwa Simba Day. Siku hiyo, wachezaji wote waliosajiliwa watatambulishwa rasmi na kutakuwa na mechi ya kirafiki kati ya Simba na SC Villa ya Uganda. Vilevile Simba SC (U-20) watavaana na African Lyon (U-20).

Ikumbukwe kuwa globu hii iliwahi kuongelea suala la kuwa na jezi za msimu ili kusaidia kuinua mapato ya klabu na morali ya wachezaji wakati wa mechi. Tunaamini huu utakuwa mwanzo mzuri na miaka ijayo badala ya kuwa na Simba Day tuwe na Simba Tournament ambapo walau timu 2 bora za West / North Africa zitakuwa zikija TZ kucheza tournament na Simba pamoa na timu nyingine teule.

Thursday, July 16, 2009

Mgosi Kumfuata Henry Joseph Norway?

Musa Hassan Mgosi(pichani), mshambuliaji wa Simba na Taifa Staz, ambae ni mchezaji pekee wa Tanzania aliyechgauliwa timu ya Africa ya mashindano ya CHAN (best 16) ameitwa kwenda Norway kufanya majaribio katika timu ya Konsvinger ya huko. Ikumbukwe timu hiyo ndio imemsajili Henry Joseph wa Simba wiki 3 zilizopita. Mgosi anatazamiwa kuondoka tarehe 25 july. Kila la Kheri Mgosi.

Kocha Phiri arudi toka Zambia,mazoezi kuanza rasmi

Kocha wa Simba, Mzambia Patrick Phiri amerejea Dar es salaam leo na kukata kidomo domo cha wanaoiombea simba mabaya ambao kila siku walikuwa wakipiga kelele kuwa Phiri harudi tena. Phiri, kocha aliyewahi kuiongoza timu ya taifa ya Zambia mara 2 katika mashindano ya CAN, ametangaza kuwa mazoezo yataanza rasmi kesho hapa hapa Dar es salaam kuiandaa na ligi ya bara inayoanza tarehe 23 august.Uwanja wa ndege alipokelewa na viongozi wa simba na kundi la ushangiliaji la kidedea.

Wednesday, July 8, 2009

Hatimae Henry Joseph asaini Norway

Baada ya sintofahamu ya muda mrefu, Henry Joseph kiuongo wa Simba amesign contract ya miaka 4 na klabu ya Konsvinger ya Norway kwa dau ambalo halijawekwa wazi (undisclosed fee). Vilevile habari nlizonazo ni kuwa mchezaji mwenzie wa Simba, Mnigeria Emeh Izechukwu ataondoka muda wowote kwenda kusign mkataba kwakuwa sasa amefikisha umri a miaka 18 ambao ndio kilikuwa kikwazo.
Wazo langu nadhani ingekuwa vizuri viongozi wangeweka wazi dau walilopata wachezaji hawa kuepuka matatizo yaliyotokea wakati wa kumuuza Odhiambo kwenda APR. Mambo ya undisclosed fee huku kwetu ambako management haiko organized sidhani kama yanajenga.