Thursday, April 30, 2009

Harakati za usajili zaanza!

Simba imeanza harakati za usajili wa wachezaji kwa ajili ya msimu ujao huku panga likielekea kuwapitia baadhi ya wachezaji wakiwamo Wanigeria Emeh Izichukwu na Orji Obinna.
Habari za uhakika kutoka ndani ya klabu zinasema, wengine walioko katika hatari ya kupitiwa na mchujo huo ni beki mzoefu Ramazan Wasso na kipa Amani Simba.

Simba imeamua kuwa msimu ujao inataka kusajili wachezaji wachache ambao watalipwa vizuri na kuachana na tabia ya kuwa na wachezaji wengi ambao hawatumiki na badala yake wamekuwa wakikaa benchi kwa msimu mzima.

Habari toka klabuni zinasema, wachezaji wengi wa msimu uliopita hasa wale nyota wamekuwa wakivurunda katika mechi nyingi na nia yao ni kuwapunguza na kumwachia kocha Patrick Phiri kusajili kikosi ambacho kitaleta mabadiliko.

Comments; Mi nadhani ule wakati wa viongozi / wafahili kusajili kila mtu mchezaji wake umepitwa na wakati. Kocha aamue anataka wachezaji gani, timu itafute pesa wasajiliwe.Sio ooh, huyu mchezaji wa kundi hili, huyu kaletwa na fulani...hapo hatujengi, tunabomoa timu. Halafu foreign player akisajiliwe awe na vitu tofauti na wa ndani, sio mtu kama Wasso!

Tuesday, April 28, 2009

Jamaa walipoponea tundu la sindano

Redondo akishangilia goli la kwanza alilowafunga Yanga katika mechi ya marudiano. Bahati yao refa aliwabeba kwa kuwaongezea dakika 7.

Juma Kaseja arudishwe Simba

Kama habari kuwa viongozi wa Simba wakiongozwa na Friends of Simba wana mpango wa kumrudisha tena Juma Kaseja Msimbazi. Je?Kuna umuhimu wa kutumia pesa nyingi kumsajili Juma? maana kwa sasa Ally Mustapha na Deo Dida ni makipa wazuri na wana uwezo wa kuendelea kuwa bora zaidi. Mi nadhani tungetumia pesa kusajili forward mmoja mzuri na attacking mid fielder badala ya kipa, wengine mnaonaje?

Monday, April 27, 2009

Phiri atupeleka CAF

Kama alivyoahidi alipofika, Coach Patrick Phiri ametimiza lengo lake kwa kutupeleka mashindano ya CAF kwa kupata nafasi ya pili. Ikumbukwe kuwa alikuja tukiwa tumepoteza points nyingi sana mzunguko wa kwanza. Pata habari kamili

Simba Yairarua Polisi Dodoma 2 - 0

Kwa matokeo hayo Simba sasa imekata tiketi ya kushiriki michuano ya Kombe la Shirikisho barani Afrika (CAF), mwakani baada ya kufikisha pointi 40, huku Yanga ambayo jana pambano lao lilishindikana kufanyika kutokana na Uwanja wa Uhuru kujaa maji ikiwa mabingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom.Hadi kipindi cha kwanza kinamalizika, hakuna timu iliyoweza kuona lango la mwenzake licha ya mpira kuwa wa kasi kubwa, huku timu zote zikishambuliana kwa zamu.Kipindi cha pili kilianza kwa kasi, huku Simba ikishangiliwa na umati wa mashabiki waliokuwa wamefurika uwanjani hapo, katika dakika ya 70, alikuwa ni Haruna Moshi 'Boban' aliyeanza kuwanyanyua mashabiki wa Wekundu wa Msimbazi kwenye viti baada ya kupachika bao safi.Baada ya dakika 12 baadaye, alikuwa ni Mohammed Kijuso aliyeihakikisha Simba kushiriki michuano ya CAF mwakani baada ya kuiandikia bao la pili na la ushindi, huku Polisi Dodoma ikikata tiketi ya kushuka daraja.Mara baada ya mchezo huo kumalizika, Katibu Mkuu wa Chama cha Mkoa wa Singida (SIREFA), Hussein Mwamba, aliliambia gazeti hili kuwa, Simba itaondoka Dodoma (Jumatatu) leo, kuelekea Singida kwa ajili ya kucheza mechi moja ya kirafiki dhidi ya Timu ya Mkoa huo, Singida Shooting Stars

Karibuni

Karibuni mashabiki na wapenzi wote wa timu ya Simba Sports Club 'Mnyama' tupashane habari, kubadilishana mawazo na hata kukosoana katika blog yetu.