Kama alivyoahidi alipofika, Coach Patrick Phiri ametimiza lengo lake kwa kutupeleka mashindano ya CAF kwa kupata nafasi ya pili. Ikumbukwe kuwa alikuja tukiwa tumepoteza points nyingi sana mzunguko wa kwanza. Pata habari kamili
Simba Yairarua Polisi Dodoma 2 - 0
Kwa matokeo hayo Simba sasa imekata tiketi ya kushiriki michuano ya Kombe la Shirikisho barani Afrika (CAF), mwakani baada ya kufikisha pointi 40, huku Yanga ambayo jana pambano lao lilishindikana kufanyika kutokana na Uwanja wa Uhuru kujaa maji ikiwa mabingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom.Hadi kipindi cha kwanza kinamalizika, hakuna timu iliyoweza kuona lango la mwenzake licha ya mpira kuwa wa kasi kubwa, huku timu zote zikishambuliana kwa zamu.Kipindi cha pili kilianza kwa kasi, huku Simba ikishangiliwa na umati wa mashabiki waliokuwa wamefurika uwanjani hapo, katika dakika ya 70, alikuwa ni Haruna Moshi 'Boban' aliyeanza kuwanyanyua mashabiki wa Wekundu wa Msimbazi kwenye viti baada ya kupachika bao safi.Baada ya dakika 12 baadaye, alikuwa ni Mohammed Kijuso aliyeihakikisha Simba kushiriki michuano ya CAF mwakani baada ya kuiandikia bao la pili na la ushindi, huku Polisi Dodoma ikikata tiketi ya kushuka daraja.Mara baada ya mchezo huo kumalizika, Katibu Mkuu wa Chama cha Mkoa wa Singida (SIREFA), Hussein Mwamba, aliliambia gazeti hili kuwa, Simba itaondoka Dodoma (Jumatatu) leo, kuelekea Singida kwa ajili ya kucheza mechi moja ya kirafiki dhidi ya Timu ya Mkoa huo, Singida Shooting Stars
Monday, April 27, 2009
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment