Tuesday, May 26, 2009

J.Kaseja huyoo Msimbazi tena

Blog hii imefahamishwa kwamba Juma Kaseja amesaini kuchezea Simba msimu ujao. Kaseja (pichani akisaini mkataba wa kuchezea Yanga mwaka jana) amekubali kuchezea Simba si kwa sababu ya pesa alizopewa tu, bali pia kutokana na mapenzi aliyonayo kwa timu hii. Ieleweke kuwa usajili wa mwaka huu zimeongezeka timu 2 zinazotumia pesa nyingi katika usajili, Azam (Ya Bakhresa) na African Lyon (Ya Moh'd Enterprises) ambazo zote zilikuwa zikimtaka kaseja pia. Katika hatua nyingine, Mganga wa tiba Asili (Maji Marefu) amejitolea kumlipa Kaseja 1.5M kama mshahara kila mwezi.

Thursday, May 21, 2009

Usajili

Timu ya Simba imetangaza rasmi kutumia Sh. Milioni 200 kwa ajili ya usajili wa msimu wa 2009 / 10. Usajili huo utajumuisha wachezaji 7 wapya. Kikosi kizima kitakuwa na jumla ya wachezaji 25. Kufuatana na uamuzi wa coach, timu itasajili kipa (1), Centre back (2), Midfielder (3) na mshambuliaji (1).
Katika hatua nyingine, wachezaji Henry Joseph na Emeh Izechukwu watauzwa Kwa timu ya FC Molde ya Norway mapea mwezi ujao.

Tuesday, May 19, 2009

Ukiona Kobe kainama......

Baada ya kuinama kwa miaka 3, sasa huu ni msimu wa Simba S.C, lazima tutambe Tanzania na Africa.

Jezi za Mwaka

Hivi sasa timu za Uingereza zimeanza kuonyesha jezi zao watakazotumia msimu ujao wa ligi. Mauzo ya jezi ni moja ya chanzo kizuri tu cha kipato kwa timu za Ulaya. Hivi kwani timu yetu ya Simba inashindwa nini kutengeneza jezi za mwaka mzima zitakazotumika na timu yetu halafu ziwepo na jezi za washabiki? Mbona Taifa Stars wanaweza sasa hivi?Mdhamini ambae tunaweka tangazo lake anajulikana, sasa tatizo ni nini?Mbona za Taifa stars zinanunuliwa, kwa nini tusijaribu?

Hivi karibuni ntawawekea jezi ambazo wajanja wanaziuza mjini zikiwa na nembo ya Simba S.C.

Thursday, May 14, 2009

Ni muhimu kujua

Kwamba Jengo la makao makuu ya klabu ya Simba (liko ktk archive ya blog hii) lililoko Msimbazi lilifunguliwa na Rais wa kwanza wa Zanzibar, Hayati Sheikh Abeid A. Karume tarehe 31 july 1971. Siku hii ndipo jina la Simba lilianza kutumika rasmi badala ya Sunderland kufuatia agizo la serikali kupiga marufuku utumiaji wa majina ya timu za kigeni kwa vilabu vya hapa nchini. wakati huo mwenyekiti wa Sunderland / Simba alikuwa ni marehemu Ramadhan Kirundu, ambaye pia alikuwa meya wa Dar es salaam.
?Hivi hili agizo la kutokuiga majina lilifutwa na nani?mbona siku hizi timu ziko kibao na majina hayo?

Tuesday, May 12, 2009

Kitega uchumi cha Simba

Jengo la kitega uchumi la Simba lililopo pembeni mwa makao makuu. Huu ni mmoja ya mfano wa mawazo ya ubunifu ambao viongozi wanatakiwa kuwa nayo kujiepusha na klabu kuwa omba omba. Jengo hili lilijengwa kwa mkataba na mfanyabiashara mmoja kufuatia wakati wa uongozi wa Kassim Dewji

Sunday, May 10, 2009

Pengo la Boban laonekana Taifa Stars

Pengo la Mshambuliaji wa Simba Haruna Moshi 'Boban' jana lilijidhihirisha wazi wakati Stars walipokuwa wakicheza na DRC na kufungwa 2 - 0. Stars waliotawala muda mrefu wa kipindi cha kwanza walishindwa kabisa kupenyesha mipira kwa mshambuliaji wa mwisho, kazi ambayo ilikuwa ikifanywa na Boban. Nizar Khalfan aliyecheza no.10 kuziba pengo la Boban alishindwa kabisa kuonyesha uwezo mkubwa hata akatolewa na nafasi ya yake kuchukuliwa na Musa Mgosi.

Wakati huo huo, mchezaji wa Simba Jabir Aziz alipata nafasi ya kucheza mechi yake ya kwanza kwa Taifa Stars na kuonyesha uwezo mkubwa. Jabir aliingia nafasi ya pili kuchukua nafasi ya Nurdin Bakari. Viongozi wa Simba wafanye kila juhudi kuhakikisha mchezaji huyu anabaki kuchezea Simba kwani ni hazina kubwa.

Thursday, May 7, 2009

Kikosi cha kutisha cha Simba

Hii ni timu ya Simba mwanzoni mwa miaka ya 90. Ikumbukwe 1993 chini ya Kibaden ndipo Simba iliingia fainali ya Kombe la CAF na kutoka suluhu katika mechi ya Kwanza ya Final kule Abidjan!Wa pili kulia aliyesimama ni Mohamed Mwameja, mwanzilishi wa jina la Tanzania One, alilopea kutokana na umahili wake

Wednesday, May 6, 2009

Simba, TFF wakwaruzana

Simba imeingia katika mzozo na TFF baada ya kuwakataza wachezaji wake wasishiriki mashindano ya mikoa (TAIFA cup). Viongozi wa Simba wanasema wamewapa wachezaji wao likizo ya mwezi mmoja kwa kuwa mwezi wa sita kutakuwa na mashindano ya Tusker, mwezi wa saba Kagame Cup na mwezi wa nane msimu wa ligi 2009 / 10 unaanza. Hivyo kama wachezaji watashiriki Taifa cup, ina maana hawatapumzika kwa mwaka mzima! TFF inalazimisha kuwa mchezaji ambae ataitwa na mkoa wowote akatae kwenda atapata adhabu kali!.
Nani yuko sahihi?mbona ukweli uko wazi?

Tuesday, May 5, 2009

Fununu za Usajili

Kuna fununu kuwa beki wa kutegemewa wa Taifa Stars na Yanga, Shadrack Nsajigwa yuko katika hatua za mwisho kabisa kuhamia Simba. Ikumbukwe kuwa misimu 2 iliyoisha, aliwahi kufungiwa miezi 6 na timu yake eti kwa kuwa alifungisha makusudi siku ya Simba.Alitaka kuhama mwaka jana lakini akaamua kumalizia mkataba wake uliokuwa umebakiza mwaka mmoja.

Makao makuu Msimbazi

Jengo la makao makuu ya Simba linavyoonekana kwa sasa.Kwa kweli hali yake hairidhishi ukilinganisha na hadhi ya timu, wakati umefika kwa viongozi kuonyesha ubunifu kusaka hela za kulikarabati na sio kusubiri wafadhili wajitokeze. mbona namna za kupata fedha ziko nyingi tu?Mahali lilipo ni kitega uchumi tosha kabisa.

Monday, May 4, 2009

Kikosi Cha Simba 2008 / 09

Kipa: Ally Mustapha*, Deo Mushi*, Amani Simba
Beki: Salum Kanoni, Juma Jabu, Ramadhan Chollo, Ramadhan wasso, Juma Nyoso, Kelvin Yondani*,Meshack Abel*, Deo Naftari, Victor Costa.
Viungo: Henry Joseph*, Nico Nyagawa (capt.), Jabir Aziz*, Haruna Moshi*, Ulimboka Mwakingwe, Ramadhan Chombo
Washambuliaji: Mussa Mgosi*, Moh’d Kijuso, Emeh Izechukwu (Nigerian), Orji Orbinna (Nigerian), Moses godwin

* - walioitwa karibuni katika timu ya Taifa

Sunday, May 3, 2009

Dewji akata mzizi wa fitna

Hatimae mwenyekiti wa kamati ya Usajili ya Simba, Kassim Dewji ameweka wazi kuwa hawatakuwa tayari kumsajili tena kipa JUma Kaseja, bali watawaendeleza waliopo sasa kwa kuwa wana uwezo mkubwa." Tumeamua kumwachia mwalimu Phiri achague wachezaji wote anaotaka kuwasajili na sisi tunachofanya ni kumpa mapendekezo tu. Lakini atakapoleta suala la Kaseja tutamwambia NO".
Pengine maoni ya wadau wa globu hii yamechangia kufikisha ujumbe kwa viongozi, tukaze kamba kuendelea kushauriana kwa manufaa ya timu yetu

Special kwa Mdau wa Ughaibuni

Kikosi cha Simba kilichoshika nafasi ya pili katika msimu huu 2008/09/ Mwenye suti ndiye Coach mkuu Patrick Phiri.Bahati mbaya timu zetu hazina utamaduni wa kupiga picha ya pamoja na wachezaji wote waliosajiliwa ktk msimu n kuziuza.Hii ingeweza hata kuongeza kipato kidogo.

Saturday, May 2, 2009

Basi za TBL


Mwenyekiti wa Simba akipokea mabasi toka kwa Mkurugenzi wa masoko wa TBL, D.Minja.

Friday, May 1, 2009

TBL waikabidhi Simba Sc. Mabasi 2

Mdhamini mkuu wa timu ya Simba, TBL kupitia bia yake ya Kilimanjaro leo wamewakabidhi Simba Mabasi 2 (Toyota Coaster 'mayai' na Toyota Hiace) kwa ajili ya matumizi ya shughuli za club!Kwa ujumla mabasi hayo yana thamani ya karibia Milioni 100 (kwa mujibu wa wadhamini).
Picha za mabasi hayo zitatoka soon! Watani wetu nao wamepewa mabasi kama sisi
Asante TBL

Fununu za Usajili

Kuna fununu kuwa Simba imemnasa kiungo wa kulia wa Yanga, Shamte Ally katika usajili wake. Habari hii bado ni fununu na haijathibitishwa na uongozi wala mchezaji mwenyewe.

Kaduguda amwaga cheche

Akizungumza na waandishi wa habari jana, Katibu Mkuu wa klabu hiyo Mwina Kaduguda (pichani), alisema kuwa uongozi wao umejipanga kuhakikisha timu inarudisha makali yake kama ya mwaka 2003 na kufikia hatua za juu za michuano ya kombe la Shirikisho. Kaduguda, alisema kuwa Simba ndio timu pekee yenye uwezo wa kufanya vizuri kwenye michuano ya kimataifa hapa nchini, ambapo rekodi yake haijawahi kuvunjwa.


"Tumeshindwa kuiwakilisha nchi kwa zaiaid ya mwaka mmoja, kipindi tulichokuwa nje kimetufundisha mengi, nina imani tutarudi na nguvu mpya,"alisema Kaduguda

Comment: Tunawatakia viongozi wetu kila la Kheri

Simba Vs Zanzibar Heroes Kesho

Timu ya Simba kesho itajipima na timu ya taifa ya Zanzibar, Zanzibar Heroes katika mchezo ulioandaliwa na TASWA. Ikumbukwe kuwa awali Simba ilipangwa kucheza na wachezaji wa nje ya TZ wanaocheza ligi kuu lakini wachezaji hao wanaoongozwa na wachezaji wengi wa Yanga wameingia mitini. Simba itakipiga bila wachezaji wao wote nyote walioko kambini na timu ya Taifa.
Kila la Kheri

Phiri kusaka vipaji mikoani

Kocha mkuu wa Simba, Mzambia Phiri amesema atazunguka nchi nzima kusaka wachezaji wa kukiongezea makali kikosi cha Simba.

“Nitazunguka mikoa mingi ya Tanzania ili kupata wachezaji watakaoweza kuisaidia timu yangu kucheza msimu ujao kwa ufanisi, si kwamba sina wachezaji mahiri...ukweli ni kwamba nataka kuwa na timu bora zaidi,” Alisema Phiri.

Comments: Hivi hatujafikia wakati wa kutumia Scouts kusaka wachezaji mikoani wakamletea kocha akawafanyia majaribio?Hata tukiamua kumlipa commission kidogo yule ambae mchezaji wake atasajiliwa, nadhani itasaidia sana. Halafu klabu yetu iimarishe timu ya vijana, sio kuokoteza wachezaji.tuyatumie mashindano ya Copa Cocacola kusajili timu imara ya vijana ambao tutawasajili na hata kuwauza nje kwa kuwa umri wao unaruhusu.