Tuesday, June 30, 2009

USAJILI SIMBA HUU HAPA / HENRY KUSIGN 2 YRS NORWAY

Baada ya pilika pilika za usajili zilizojaa kila aina ya maneno, hatimae blogu ya wapenzi imefanikiwa kupata majina ya wachezaji waliosajiliwa Simba kwa ajili ya msimu 2009 / 10, ambao ni; Juma Kaseja, Danny Mrwanda (alikuwa Kuwait kwa miaka 2), Zahoro Pazi, Uhuru Seleman (Mtibwa), Amri Kiemba (Moro United), Salim Aziz (Tanga), Hillary Echesa (Kenya) na Emmanuel Okwi (Nigeria).Dany, Zahoro na Uhuru ni wachezaji wa timu ya Taifa ya Tanzania. Juhudi bado ziko mbioni kumnasa kiungo anayeng'ara kwa sasa Mwinyi Kazimoto toka JKT (Huyu ndiye aliwafunga New Zealand goli kama la Iniesta)

Habari zingine zinasema, Henry Joseph huenda akasaini mwisho wa wiki hii mkataba wa miaka 2 na timu ya Kongsvinger ya Norway (Mdau wa Norway anaweza kutusaidia hili maana labda hata magazeti ya ki Nolsk yatakuwa yameandika)

Wednesday, June 10, 2009

Uongozi Simba huu utoto sasa

Wikiendi hii uongozi wa Simba ulishindwa kumpata katibu mkuu wa kuajiriwa baada ya kutokea ugomvi katika kikao cha kamati ya utendaji kilichotakiwa kumpitisha Katibu huyo. Chanzo inasemekana ni baadhi ya wajumbe kumkataa Kaduguda, ambae inasemekana ndiye aliyeongoza katika usaili uliofanywa na kamati ya usaili. Huu mi naona ni utoto na ufinyu wa mawazo kwa viongozi wetu. Hii yote ni kutokana na kutanguliza ubinafsi badala ya maslahi ya timu. Hivi kwanini msiiamini kamati ya usaili iliyoundwa na mwenyekiti ambayo imejaa wasomi na kuongozwa na wakili aliyebobea katika sheria?kana haja gani ya kuanza kujadili tena majina yaliyopitishwa na kamati mliyoiamini wenyewe?Hamuoni mnawavunjia heshima mliowateua ktk kamati ya usaili? Kama mmeshindwa kutokana na ubinafsi wenu si bora muwape kazi hiyo recruitment agencies kama Radar, My goli au zingine wawasaidie kufanya usaili?swali linakuja,je wakichagua watu ambao sio mnalazimisha nyie washinde mtawakubali? acheni ubinafsi kuepusha simba isije ikazuiliwa kushiriki ligi kuu inayoanza Agosti.

Monday, June 8, 2009

Henry Joseph kwenda Norway Leo


Kiungo wa kutumainiwa wa Simba, Henry Joseph Shindika, anaondoka leo kwenda Norway kuanza mpira wa kulipwa katika timu ya Kongsvinger iliyoko daraja la Kwanza. Henry ataongozana na Mnigeria, Emeh Izehukwu wa Simba ambao kwa pamoja walionekana walipokwenda kufanya majaribio katika klabu ya FC Molde huko Norway ambako hawakufuzu, lakini wakaonwa na wakala wa timu ya Kongsvinger ambae aliwapeleka katika timu hiyo. Ikumbukwe timu hii ya Norway ambayo ndio inaongoza ligi kwa sasa, majuzi wali sign mkataba wa ushirikiano na timu iliyopanda ligi kuu hapa Tanzania ya African Lyon ambao watakuwa wakibadilishana ufundi, rasilimali na wachezaji. Pichani Henry akicheza mechi ya mwisho kwa timu ya Simba dhidi ya African Lyon.

Thursday, June 4, 2009

Simba kuajiri katibu mkuu Jmosi

Klabu ya Simba jumamosi hii itaweka historia kwa kuwa na katibu mkuu aliyeajiriwa kwa mara ya kwanza tangu kuanzishwa kwa timu hiyo. Uamuzi huo unafuatia maagizo ya TFF / FIFA yanayotaka timu zote zinazoshiriki ligi kuu kuwa na katibu mkuu na Mhazini mwenye ujuzi aliyeajiriwa. Waliopita mchujo na hivyo kushiriki ktk interview ya jumamosi ni Mwina Kaduguda, Michael Maurus na Hamisi Kisiwa. Wagombea hao wote wana degree angalau moja. Blogu hii ya mashabiki inawatakia kila mafanikio wagombea na yeyote atakaeshinda atumie nafasi hiyo kuendeleza Simba.

Monday, June 1, 2009

Mchezaji bora wa Taifa Cup atua Msimbazi

Salum Aziz wa Tanga, ambae ametangazwa mchezaji bora wa mashindano ya Kili Taifa Cup iliyomalizika karibuni, amejiunga na wekundu wa Msimbazi. Habari za ndani zinasema Salum amesaini mkataba wa miaka 2 huku gharama ya mkataba ikiwa ni siri. Wakati huo huo mchezaji mkongwe Ulimboka Mwakingwe ameishauri kamati ya usajili kuchanganya na wachezaji wazoefu katika usajili ili kufanya vizuri tangu mwanzo mwa msimu.