Wednesday, June 10, 2009

Uongozi Simba huu utoto sasa

Wikiendi hii uongozi wa Simba ulishindwa kumpata katibu mkuu wa kuajiriwa baada ya kutokea ugomvi katika kikao cha kamati ya utendaji kilichotakiwa kumpitisha Katibu huyo. Chanzo inasemekana ni baadhi ya wajumbe kumkataa Kaduguda, ambae inasemekana ndiye aliyeongoza katika usaili uliofanywa na kamati ya usaili. Huu mi naona ni utoto na ufinyu wa mawazo kwa viongozi wetu. Hii yote ni kutokana na kutanguliza ubinafsi badala ya maslahi ya timu. Hivi kwanini msiiamini kamati ya usaili iliyoundwa na mwenyekiti ambayo imejaa wasomi na kuongozwa na wakili aliyebobea katika sheria?kana haja gani ya kuanza kujadili tena majina yaliyopitishwa na kamati mliyoiamini wenyewe?Hamuoni mnawavunjia heshima mliowateua ktk kamati ya usaili? Kama mmeshindwa kutokana na ubinafsi wenu si bora muwape kazi hiyo recruitment agencies kama Radar, My goli au zingine wawasaidie kufanya usaili?swali linakuja,je wakichagua watu ambao sio mnalazimisha nyie washinde mtawakubali? acheni ubinafsi kuepusha simba isije ikazuiliwa kushiriki ligi kuu inayoanza Agosti.

1 comment:

  1. Kweli kabisa,tatizo timu zetu zinaongozwa na watu wenye uwezo mdogo wa kutawala,ndio maana wanayumbishwa na watu wachache. mwenye akili ameelewa

    ReplyDelete