Tuesday, June 30, 2009

USAJILI SIMBA HUU HAPA / HENRY KUSIGN 2 YRS NORWAY

Baada ya pilika pilika za usajili zilizojaa kila aina ya maneno, hatimae blogu ya wapenzi imefanikiwa kupata majina ya wachezaji waliosajiliwa Simba kwa ajili ya msimu 2009 / 10, ambao ni; Juma Kaseja, Danny Mrwanda (alikuwa Kuwait kwa miaka 2), Zahoro Pazi, Uhuru Seleman (Mtibwa), Amri Kiemba (Moro United), Salim Aziz (Tanga), Hillary Echesa (Kenya) na Emmanuel Okwi (Nigeria).Dany, Zahoro na Uhuru ni wachezaji wa timu ya Taifa ya Tanzania. Juhudi bado ziko mbioni kumnasa kiungo anayeng'ara kwa sasa Mwinyi Kazimoto toka JKT (Huyu ndiye aliwafunga New Zealand goli kama la Iniesta)

Habari zingine zinasema, Henry Joseph huenda akasaini mwisho wa wiki hii mkataba wa miaka 2 na timu ya Kongsvinger ya Norway (Mdau wa Norway anaweza kutusaidia hili maana labda hata magazeti ya ki Nolsk yatakuwa yameandika)

3 comments:

  1. Wapi Jabir Aziz?

    ReplyDelete
  2. Hawa ni wachezaji wapya waliosajiliwa kwa ara ya kwanza mwaka huu. Kifaa Jabir Aziz bado yuko Msimbazi na ataendelea kukipiga Simba kwa mwaka mwingine tena

    ReplyDelete
  3. bado cjackia makeke ya casilas




    ReplyDelete