
Kiungo wa kutumainiwa wa Simba, Henry Joseph Shindika, anaondoka leo kwenda Norway kuanza mpira wa kulipwa katika timu ya Kongsvinger iliyoko daraja la Kwanza. Henry ataongozana na Mnigeria, Emeh Izehukwu wa Simba ambao kwa pamoja walionekana walipokwenda kufanya majaribio katika klabu ya FC Molde huko Norway ambako hawakufuzu, lakini wakaonwa na wakala wa timu ya Kongsvinger ambae aliwapeleka katika timu hiyo. Ikumbukwe timu hii ya Norway ambayo ndio inaongoza ligi kwa sasa, majuzi wali sign mkataba wa ushirikiano na timu iliyopanda ligi kuu hapa Tanzania ya African Lyon ambao watakuwa wakibadilishana ufundi, rasilimali na wachezaji. Pichani Henry akicheza mechi ya mwisho kwa timu ya Simba dhidi ya African Lyon.
Mzee mimi ni Simba kama wewe, naona vyombo vya habari vinapotosha ukweli, Henry haji kucheza soka la kulipwa bali anakuja kufanya majaribio baada ya kushindwa kufuzu majaribio ya awali na Molde. Mimi nipo hapa Norway nafuatilia kwa karibu sana habari hizi. Nafahamu hata wakala wa Henry alisema kuwa Henry anakuja kufanya majaribio. Nimeona niseme hili sababu ya kuna habari nyingi sana za kupotosha na nimekuwa napata emails nyingi kwa watu juu ya hili. Haya usajili vipi huko?
ReplyDeleteAsante sana mdau wa Norway, nadhani hilo hata viongozi wengine hawajui, maana mpaka hela ya uhamisho wameshanitajia. Norway uko Oslo, nilikaa Bergen 6 months! Usajili huku ni mkanganyiko, maana majina yanatajwa lakini habari za ndani zinasema hela hakuna.Source ikinipa habari ntawapasha
ReplyDelete