Wednesday, July 8, 2009

Hatimae Henry Joseph asaini Norway

Baada ya sintofahamu ya muda mrefu, Henry Joseph kiuongo wa Simba amesign contract ya miaka 4 na klabu ya Konsvinger ya Norway kwa dau ambalo halijawekwa wazi (undisclosed fee). Vilevile habari nlizonazo ni kuwa mchezaji mwenzie wa Simba, Mnigeria Emeh Izechukwu ataondoka muda wowote kwenda kusign mkataba kwakuwa sasa amefikisha umri a miaka 18 ambao ndio kilikuwa kikwazo.
Wazo langu nadhani ingekuwa vizuri viongozi wangeweka wazi dau walilopata wachezaji hawa kuepuka matatizo yaliyotokea wakati wa kumuuza Odhiambo kwenda APR. Mambo ya undisclosed fee huku kwetu ambako management haiko organized sidhani kama yanajenga.

2 comments:

  1. Kwanza nashukuru sana kwa blog hii, inatusaidia sana hasa sisi wapenzi wa Simba tuliopo nje ya Tanzania. Mimi nipo Norway, ukweli ni kuwa Soka la hapa siyo juu sana kama wakala alivyosema. Kuhusu ada ya uhamisho wa Henry Joseph, nadhani siyo dau kubwa sana, sababu hapa mchezaji anayelipwa kwa mshahara wa juu ni Euro 2,000 kwa wiki. Nadhani Henry Joseph atakuwa analipwa something like 1800 to 1500 Euro kwa wiki, nitafuatalia hili nakuwajulisha.

    ReplyDelete
  2. Tutashukuru sana mdau ukitupa taarifa kamili. Habari zilizoko huku ni kuwa Henry anapokea USD 260,000 kwa mwaka. Nakubaliana na wewe kuwa Norway mpira wao hauko juu sana, mwaka jana nilihudhuria mazoezi na mechi 2 za Brann FC ya Bergen uwanjani kwao, Ni kweli hawajifikia viwango vya France au Holland (ambako ndio Henry anasema ni target yake kwa sasa) lakini naamini wametuzidi Soka letu la TZ hasa unde wa technical, Physical game na discpline. Naamini Henry atakuwa na mengi ya kujifunza. Tunakutegemea wewe mdau uwe unatuletea maendeleo yake huko.SIMBA FAN NO.1

    ReplyDelete