Simba imeanza harakati za usajili wa wachezaji kwa ajili ya msimu ujao huku panga likielekea kuwapitia baadhi ya wachezaji wakiwamo Wanigeria Emeh Izichukwu na Orji Obinna.
Habari za uhakika kutoka ndani ya klabu zinasema, wengine walioko katika hatari ya kupitiwa na mchujo huo ni beki mzoefu Ramazan Wasso na kipa Amani Simba.
Simba imeamua kuwa msimu ujao inataka kusajili wachezaji wachache ambao watalipwa vizuri na kuachana na tabia ya kuwa na wachezaji wengi ambao hawatumiki na badala yake wamekuwa wakikaa benchi kwa msimu mzima.
Habari toka klabuni zinasema, wachezaji wengi wa msimu uliopita hasa wale nyota wamekuwa wakivurunda katika mechi nyingi na nia yao ni kuwapunguza na kumwachia kocha Patrick Phiri kusajili kikosi ambacho kitaleta mabadiliko.
Comments; Mi nadhani ule wakati wa viongozi / wafahili kusajili kila mtu mchezaji wake umepitwa na wakati. Kocha aamue anataka wachezaji gani, timu itafute pesa wasajiliwe.Sio ooh, huyu mchezaji wa kundi hili, huyu kaletwa na fulani...hapo hatujengi, tunabomoa timu. Halafu foreign player akisajiliwe awe na vitu tofauti na wa ndani, sio mtu kama Wasso!
Thursday, April 30, 2009
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment